KATIBU MKUU WA ZAMANI WA SIMBA ATOA TATHIMINI YA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA....ASEMA YANGA WALIIZIDI SIMBA
Katibu Mkuu wa zamani wa klabu ya Simba Mhina Kaduguda ametoa tathmini yake kuhusiana na mchezo wa watani wa jadi uliochezwa jumamosi Oktoba 28, 2017 katika uwanja wa Uhuru na kuweka wazi kuwa Yanga walicheza vizuri zaidi ya Simba.
"Mpira ulikuwa mzuri lakini Simba walikwenda na matumaini makubwa kutokana na Kikosi chao kuwa cha thamani kubwa lakini kiufundi Yanga walitawala mchezo kwa asilimia kubwa kuliko Simba, Mechi ya Juzi Yanga walitakiwa kushinda si chini ya Goli Mbili, Emmanuel Martin alikosa Goli la Wazi,Mwashiuya alipoteza nafasi nzuri ya Kufunga, Ajibu kuna mpira aliunganisha moja kwa moja angeweza kuuweka kifuani na kuushusha chini akaupress akafunga goli"
Kaduguda pia amepigia msumari kwa kusema kama angetoa Takwimu basi angewapa Yanga asilimia 60 na Simba angewapa asilimia 40.
"Kama asilimia Yanga ningewapa 60 Simba Ningewapa 40, Ngoja Niseme Ukweli Simba ni timu yangu lakini mimi ni kocha lazima niseme ukweli Yanga walicheza vizuri zaidi"
Katika mchezo huo SIMBA na YANGA zilimaliza mchezo huo kwa sare ya bao 1 kwa 1 magoli yakifungwa na Shiza Kichuya dakika ya 58 na Yanga wakachomoa kupitia kwa Obrey Chirwa dakika 3 baadaye dakika ya 61.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi