HALIMA MDEE AMTAHADHARISHA LAZARO NYALANDU KUHUSU CHADEMA

Mbunge wa Kawe jijini Dar es salaam, Halima Mdee amemkaribisha na kumtahadharisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akimtaka ajiandae kisaikolojia kupambana na changamoto wanazokumbana nazo viongozi wa Chadema.

Ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter kumkaribisha ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mara baada ya kutangaza kukihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiuzulu nafasi ya Ubunge.

“Mhe. Nyalandu karibu sana CHADEMA. Naamini utakuwa imara kukabiliana na siasa za chuki, ubaguzi na visasi zinazolikabili taifa letu, hivyo naimani umechukua maamuzi mazuri ila jiandae kukabiliana na changamoto,”amesema Mdee

Jana Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri ya Kamati Kuu CCM alitangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kwamba hafurahishwi na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kupitia chama hicho.


Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.