HABARI MPYA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE KUTOKA KLABU YA YANGA
Mara baada ya kumaliza mchezo wa raundi ya 8 kati yao na watani wa jadi Simba Klabu ya Yanga leo itafanya mazoezi katika uwanja wa Uhuru mara baada ya siku ya jana kufanya mazoezi ya GYM hii ni kulingana na Taarifa iliyotoewa na Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano klabu ya Yanga Dismas Ten.
Yanga inajiandaa na mchezo wa Raundi ya 9 Wa raundi ya 9 ligi kuu soka ya Tanzania Bara VPL dihdi ya Singida United 4 November 2017.
Singida United watakuwa wenyeji wa mchezo huo na kwa mara ya kwanza Singida United watakuwa wakiutumia uwanja wao wa Nyumbani Namfua Stadium uliokuwa umefungwa kwa marekebisho ya Pitch na sehemu nyingine za uwanja.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi