GOLIKIPA WA SIMBA AISHI MANULA AFUNGUKA KUHUSU MASHUTI YA TSHISHIMBI YALIVYOMTESA


Kipa namba moja wa klabu ya Simba Sc na timu ya taifa ya Tanzania , Aishi Manula amesema kuwa shuti lililopigwa na kiungo wa Yanga Papy Kabamba Tshishimbi katika mchezo baina ya timu hizo mbili kwenye uwanja wa Uhuru Juzi lilikua si la kawaida na iwapo asingekua imara basi lingeleta madhara makubwa kwake na timu kwa ujumla.

Mpira huo uliopigwa na mkongomani huyo akiwa sentimita chache nje ya mstari wa 18 mnamo dakika ya 30' ya mchezo huo na kutolewa na Mamula na hatimae kuwa jona .Ni wazi endapo zisingekua juhudi za mlindalango huyo basi yangelizumzwa mwngine.

Katika mchezo huo ambao ulikua ni wa raundi ya nane ya ligi kuu Tanzania ulikua wa aina yake kwani ulishuhudia uwezo binafsi kwa baadhi ya wachezaji ambapo wawili hao (Manuka na Tshishimbi) waling'ara kila mmoj kwa nafasi yake.

Licha ya Manula kuicheza bunduki ile kutoka kwa Tshishimbi lakini mwenyewe amekiri kuwa ni moja ya mipira mikali na iliyokua na Madhara aliyoicheza.

Mchezo huo ulimakizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa sare ya foli 1-1..

Source:Dimba

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.