BAADA YA KUONEWA KWA MUDA MREFU, TIMU YA SIMBA YACHUKUA MAAMUZI MAGUMU
Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema klabu yake imeandika barua kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe kumlalamikia baadhi ya matukio yanayozua utata yanayosababishwa na waamuzi wa ligi kuu Tanzania bara pindi Simba inapokuwa inacheza na timu nyingine.
Manara akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari amethibitisha kwamba, Simba imeandika barua kwenda TFF, Bodi ya Ligi, Chama cha Waamuzi na nakala imepelekwa kwa Waziri mwenye dhamana ya michezo (Dkt. Harisson Mwakyembe).
“Tumeandika barua TFF, Bodi ya Ligi na nakala tumempelekea Waziri mwenye dhamana ya Michezo na Chama cha Waamuzi, barua itakwenda kulalamikia matukio haya sizungumzii Yanga ndio maana nimeweka matukio yote (Mbao na Stand) mechi zote zikiwa mfululizo”-Haji Manara.
Manara analalamikia Simba kunyimwa penati kwenye mchezo dhidi ya Mbao uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza baada ya mshambuliaji wao John Bocco kuangushwa kwenye eneo la hatari (penati box) Manara pia amesema klabu yake ilinyimwa penati mbili wakati ilipocheza dhidi ya Yanga kufuatia Kelvin Yondani na Papy Tshishimbi kushika mpira kwenye eneo la hatari kwa nyakati tofauti.
Jambo jingine ambalo Manara amelipigia kelele kuhusiana na waamuzi ni klabu ya Stand kupewa penati isiyo halali kwa sababu mwamuzi alimtuhumu Ally Shomary kuushika mpira kwenye eneo la hatari lakini haikuwa hivyo
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi