HAJI MANARA AMGEUKIA TUNDU LISSU NA HIKI NDICHO ALICHOANDIKA INSTAGRAM

Sakata la mwanasheria Tundu Lisu kushambuliwa kwa risasi bado ni gumzo nchini Tanzania.

Mwanasheria huyo ambaye pia ni mbunge alikutwa na tukio hilo juzi Alhamisi alipokuwa akielekea nyumbani kwake Area D mkoani Dodoma akitokea bungeni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara naye alitoa maoni yake juu ya hicho kilichotokea.

Manara kaandika haya: “Mimi ni Mwanaccm kindakindaki na sina haya kwenye hili, ila mimi ni Mtanzania zaidi kuliko itikadi yangu, naomba uzima wa afya ya mh Tundu Lisu @tundulissutz, upone haraka bro, muhimu tuache vyombo vije kutupa uchunguzi wao.”