Klabu ya Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara imekanusha taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya Kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuwa imempa mechi 5 za kumpima kocha wake Mkuu Joseph Omog.
Simba wamesema Omog haendi popote bado ni Kocha Mkuu wa Simba na hawana mipango ya Kumfukuza kocha huyo ambaye msimu uliopita ilibaki kidogo aipe Simba Ubingwa ambao ulikwenda kwa Wapinzani wao Yanga.
Kuhusu Jonas Mkude kutopangwa katika kikosi cha Simba mechi mbili za awali Manara amesema Mkude alikuwa anaumwa Ugonjwa wa Macho anashangaa kuona washabiki kwanini walikuwa wanapiga kelele.
Manara amesema hajui washabiki wanataka Furaha gani kwani kama kushinda walishinda 7 kabla ya sare na Azam wamempiga mtu 3, Manara amesisitiza washabiki na wapenzi wa Simba kuwa watulivu.