HABARI NJEMA ZILIZOTUFIKI KUTOKA TIMU YA YANGA JIONI HII

Dar Es Salaam
Klabu Bingwa wa Mpira wa Miguu Tanzania Bara Yanga wamezidi kujiweka sawa kwa mazoezi makali kuelekea mechi kati yao dhidi ya Njombe Mji, Katika mazoezi ya jana Yanga chini ya Benchi lao la Ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu George Lwandamina na Msaidizi wake Shadrack Nsajingwa walionekana kukazia eneo la Ushambuliaji.

Benchi la ufundi msomaji wa Mkaliamngi Blog lilionekana kutumia Muda mwingi zaidi katika kuhakikisha washambuliaji wanapata mbinu zaidi katika Ufungaji, Tulipomuuliza kocha msaidizi wa Yanga Nsajingwa alisema Katika mechi ya Kwanza dhidi ya Lipuli timu ilitengeneza nafasi nyingi lakini safu yao ya Ushambuliaji ilishindwa kuwapa matokeo kulingana na nafasi hizo.

Kwahiyo ndiyo maana benchi la Ufundi limekazia zaidi kwenye safu ya Ushambuliaji ili kuhakikisha Wanafunga magoli kwenye nafasi watakazotengeneza