HABARI NJEMA KUTOKA TIMU YA YANGA ZILIZOTUFIKIA LEO JUMATATU SEPTEMBA 18, 2017

HABARI MPYA KUTOKA YANGA LEO 18.9.2017
Dar Es Salaam,
Klabu ya Yanga jana imewasili salama jijini Dar Es Salaam kutokea Songea Mkoani Ruvuma ilipokuwa inamechi ya Ligi Kuu VPL dhidi ya Maji Maji, Yanga imetoa mapumziko kwa wachezaji wake kwa Siku ya Leo.

Wachezaji watakutana kesho (Jumanne 19.9.2017) kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na Mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ndanda mechi ambayo Yanga watacheza wakiwa Nyumbani Uhuru Stadium.

Kabla ya kwenda Songea, Klabu ya Yanga ilicheza mechi dhidi ya Njombe Mji ambapo ilishinda bao 1 kwa 0 kabla ya kulazimishwa sare dhidi ya Maji Maji katika Mchezo uliopita.