SPIKA NDUGAI AFUNGUKA MAZITO BAADA YA WABUNGE KUMSHANGILIA KUPITA KIASI RAISI KIKWETE WAKATI WA KIKAO CHA BUNGE HAPO JANA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameshangazwa na jinsi wabunge walivyomshangilia Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na kuelezea kuwa hakuna mgeni aliyewahi kupata shangwe kama hizo.

Rais Mstaafu huyo ameshangiliwa kwa muda mrefu mara baada ya kuingia bungeni leo asubuhi alipoenda kumshuhudia mke wake, Mama Salma akiapishwa tangu ateuliwe kuwa mbunge.

“Waheshimiwa wabunge, binafsi mimi ni kipindi cha nne humu bungeni sijawahi kuona mgeni amepokelewa kwa kiwango hiki,” alisema Spiga Ndugai huku akicheka kwa furaha.


Ikumbukwe kuwa Bunge limeanza jana mjini Dodoma.



Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.