GABO ASEMA HAYA KUHUSU KUONJA PENZI LA WEMA SEPETU


Gabo Afunguka Kuonja Penzi la Wema Sepetu

.

KUFUATIA uwepo wa madai kuwa amelionja penzi la mwigizaji Wema Sepetu, mkali anayekimbiza kwa sasa katika soko la sinema kwa Bongo, Salim Ahmed ‘Gambo’ amebanwa na Risasi na kufungukia uhusiano wake na Wema Sepetu.

Awali, mwanahabari wetu alihakikishiwa na msanii mmoja (jina tunalihifadhi) kuwa kabla ya kuvuja kwa picha za sinema za Wema na Gabo za filamu hivi karibuni, wawili hao waliwahi kuanguka dhambini miaka kadhaa iliyopita.
“Kwani unafiri ukaribu wa Wema na Gabo ni filamu tu? Kuna zaidi ya filamu, walishawahi kutoka miaka ya nyuma na ndio maana umeona hivi karibuni imekuwa rahisi tu kwao kufanya tena kazi pamoja,” alisema msanii huyo.
Baada ya kupata ubuyu huo, mwanahabari wetu alimtafuta Wema ili kuweza kumsikia anazungumziaje ishu hiyoi lakini bahati mbaya mrembo huyo hakuweza kupokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, pia hakujibu. Alipoulizwa Gabo kuhusiana na madai hayo, alisema ukaribu wake na Wema umekuwa ukitafsiriwa tofauti lakini ukweli ni kwamba yeye wanakutanisha zaidi na kazi tu na si vinginevyo.

“Mimi si mara moja au mara mbili. Wema nakutana naye, nakuwa karibu naye kwa ajiuli ya kazi. Umeona picha mpya za kimahaba hivi karibuni, zile ni za muvi tu,” alisema Gabo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.