DIAMOND KUJENGA HOSPITALI YA MOYO TANDALE
Katika harakati za kurudisha kwa jamii kile anachokipata, mkali wa wimbo ‘Marry You’, Diamond Platnumz, ameweka wazi mpango wake wa kujenga hospitali ya moyo na magonjwa mengine katika mtaa aliozaliwa, Tandale Jijini Dar es salaam.
Muimbaji alisema tayari amefanya mazungumzo na wadau mbalimbali na wamemuahidi kumpatia vifaa kwa ajili ya hospitali hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii wakati akizindua perfume yake mpya ‘CHBU’, Diamond alisema hospitali hiyo itawasaidia Watanzania wa hali ya chini.
“Mafanikio yote tunayopata hatusahau kurudisha kwa jamii kile tunachokipata,” alisema Diamond. “Ukiachana na misikiti ambayo nimekuwa nikiijenga katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania habari nje kwa ndugu zangu wa Tandale ni kwamba nataka kuwajengea hospitali ambayo itakuwa inatoa huduma pale kwa bei nafuu,”
Aliongeza, “Kuna wadau wangu wanakaa nje, nimezungumza nao wameniambia nijenge tu nay wao kuna baadhi ya vifaa wataleta. Kwa hiyo nikaona hii ni fursa na tayari kuna baadhi ya mambo ya mwanzo tumeanza kuyashughulikia. Nataka ufike muda watu waache kwenda kusafiri nje kutibiwa magonjwa mbalimbali kama moyo na mengine ambayo yamekuwa akitufanya tusafiri nje kwa ajili ya matibabu,”
Perfume aliyozindua muimbaji huyo imeanza kuuzwa rasmi leo nchini kwa bei ya Tsh. 105000.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi