MSANII wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’, ametoa pongezi kwa mwanafamilia wa Wasafi Classic Baby (WCB), Rayvanny, kwa kupata mtoto wa kwanza.
Rayvanny na Fahyma.
Diamond amechapisha katika ukurasa wake wa Instagram ujumbe wa kumpongeza Rayvanny na mzazi mwenzake aliyefahamika kwa jina moja la Fahyma.
Mpaka sasa bado halijafahamika jina la mtoto huyo ambapo katika familia ya WCB wasanii wote wanaounda kundi hilo wana watoto isipokuwa Harmonize.

