FAIDA ZA EMBE MWILINI


Embe ni Tunda kama matunda mengine yakawaida tu, lakini ipo siri kubwa sana iliyojificha kwenye Tunda hili. Mbali kuwa inaongeza ufahamu, na kusaidia kuongeza Vitamini A, C na E. Pia Embe inasaidia...

*Huzuia Kansa:- 
Embe limebeba madini ya Polyphenols ambayo husaidia kuondoa kansa ya ziwa, utumbo, mapafu, prostate kansa na Luekemia.






*Kuboresha mmeng'enyo wa Chakula:- Embe limebeba nyuzinyuzi{Fibers} ambazo kusaidia kusaga chakula mwilini.




*Kuboresha ngozi:-Embe imebeba Vitamin A, ambayo husaidia kupambana na mapele au chunusi. Ni moja ya Tunda zuri sana kutumia kwa kuboresha ngozi yako. Vitamin C na E iliyopo kwenye Embe hulinda ngozi na miale ya jua, inayoweza kuharibu ngozi yako. 
Waweza chukua Embe lililoiva, lisage, kisha paka moja kwa moja kwenye ngozi yako kwa ajili ya kusafisha uso wako na uchafu ambao haundoki na sabuni pekee, na pia itakusaidia kufungua vijitundu vya ngozi.



*Kuboresha Kuona:- Embe imebeba Vitamini A yakutosha ambayo husaidia kuona. Hulinda jicho na matatizo yakutokuona mchana au usiku. 



*Kuboresha Hisia za kimapenzi:- Hii ni ngeni eeh? Lakini kweli. Embe ina Vitamini E, ambayo inatengeneza au huamsha hisia za mapenzi.



*Huongeza madini ya Chuma:-
Madini ya chuma yaliyopo kwenye embe husaidia kuongeza madini hayo mwilini na kusaidia upungufu wa damu mwilini. Vitamini C iliyopo kwenye embe, husaidi kuupa mwili uwezo wa kufyoza kiurahisi madini hayo ya chuma, kutoka kwenye vyakula vingine.

*Kuimarisha kinga ya mwili:- 
Kiwango kikubwa cha Vitamin A, kilichopo kwenye Embe, kinasaidia kujenga kinga ya mwili. 




*Kupunguza Cholesterol mwilini:-

Madini yaliyopo kwenye embe pamoja na Vitamin C, vyote vinasaidia kushusha cholesterol mwili.

Waweza kula embe kama lilivyo au ukatengeneza juisi yake. Vyote vinafanya kazi ile ile. 

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.