CCM YAANGUKA KESI YA UBUNGE ARUSHA
Mahakama ya Rufaa nchini imetupilia mbali rufaa ya kupinga hukumu ya kesi ya uchaguzi katika jimbo la Longido mkoani Arusha, yaliyompa ushindi Onesmo Ole Nangole (Chadema), iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Stephen Kiruswa,Uamuzi huo umesomwa leo (Alhamisi) na msajili wa Mahakama ya Rufaa nchini, Amir Msumi na kusema kwamba wakata rufaa waliwasilisha rufaa mpya badala ya kurekebisha baadhi ya vipengele kama walivyoagizwa na mahakama.
Msumi amesema badala ya kuwajumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na msimamizi wa uchaguzi kwenye rufaa hiyo, wakata rufaa walifanya kitu ambacho hawakuruhusiwa kukifanya na mahakama na hivyo rufaa hiyo imetupwa na wanapaswa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hiyo.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi