Polisi yapiga marufuku kuchoma matairi, disco toto

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo,

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limepiga marufuku uharibifu wa Miundombinu wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2017 ikiwemo uchomaji wa matairi barabarani hali ambayo husababisha usumbufu kwa Wananchi.

Marufuku hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya jinsi gani jeshi hilo lilivyojipanga katika kuhakikisha wakazi wa mkoa huo wanaingia mwaka mpya kwa amani na utulivu.

Kamanda Mkumbo amesema Jeshi hilo litashirikiana na wakala wa Barabara (TANROADS) na kuongeza kuwa yoyote atakaebainika kuchoma matairi sheria itachukua mkondo wake ikiwemo kulipishwa faini ambayo si chini ya milioni 4.

Katika hatua nyingine Kamanda huyo ametoa wito kwa wazazi kuwalinda watoto wao, huku akipiga marufuku kuwepo kwa Disco toto katika kuukaribisha mwaka mpya