PICHA: Tajiri ampiga Risasi kijana wa miaka 19 Tarime


Kutoka Tarime imeripotiwa kuwa tajiri mmoja ajulikanaye kwa Jina la Ndugu Mkazi wa sirari wilayani humo amemuua kijana mmoja (19) kwa kumpiga Risasi,

Kwa mujibu shuhuda wa tukio hilo ameuambia mtandao huu kuwa hatua hiyo imefuata baada ya wawili hao kutofautiana kauli mapema leo Leo trh 30/12/2016 majira ya SAA 7:00 mchana huko katka kijiji cha sirari wilaya ya tarime.

Baaada ya kitendo hicho wananchi wenye hasira kali waliamua kulichoma moto gari la tajiri huyo  na kutaka kuchoma moto hotel anayoimiliki Ndugu iliyopo katika mji mdogo wa sirari wilayani humo.

Polisi walitanda katika hotel hiyo huku wakiwadhibiti wananchi kwa mabomu ya machoz na Risasi za moto,  

Jamaa huyo (Ndugu) inasemekana amejisalimisha ktk kituo cha polisi sirari wilayan Tarime

TAZAMA PICHA ZA TUKIO HILO HAPO CHINI...




Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.