Newsw Alert: Mpiga picha maarufu Mpoki Bukuku afariki Dunia


Mpiga picha maarufu Mpoki Bukuku amefariki dunia leo katika Taasisi ya mifupa (MOI) alipokua amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano kwa umma (MOI) Almas Jumaa.

"Ni kweli Mpoki amefariki Dunia mchana huu, alipokelewa jana usiku baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Mwenge ITV, taarifa zaidi tutazitoa baadae."

Mpoki Bukuku amewahi kufanya kazi kamaq mpiga picha mkuu katika gazeti la Mwananchi, linalochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen  na Mwanasport. Pia amewahi kufanya kazi magazeti kadhaa ikiwamo Majira na Nipashe.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI, AMINA

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.