Baada ya kuapishwa M/kiti NEC aanza na kazi hii
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Imetangaza orodha ya walioteuliwa kugombea uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani katika majimbo na kata mbalimbali kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara, utakao fanyika tarehe 22 mwezi Januari mwaka 2017.
Akiongea na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kuapishwa na kuwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, Jaji Semistocle Kaijage amesema, jumla ya vyama 11 vimeweka wagombea, ambapo wagombea wote 11 wameteuliwa kwa jimbo la Dimani Zanzibar.
Jaji. Kaijage amesema, vyama 13 vimesimamisha wagombea wa Udiwani katika Halmashauri 20 za Tanzania Bara kukiwa na wagombea wapatao 72 ambao wameteuliwa kuwania uchaguzi huo.
Aidha, Jaji Kaijage amesema, ratiba ya kampeni ya uchaguzi huo zitaanza tarehe 23/12/2016 hadi tarehe 21/01/2016 ambapo kamati za maadili zinaundwa katika ngazi mbalimbali kwaajili ya kusimamia utekelezaji wa maadili katika kipindi chote cha kampeni.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi