ZIFAHAMU DALILI ZA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO



Hapo kabla tulisoma kwa kirefu kuhusu vidonda vya tumbo, kisha tukasoma kuhusu dawa mbadala ya vidonda vya tumbo, tukasoma tena kuhusu chakula cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo, na leo tunaendelea kuangalia dalili za ugonjwa wa vidonda vya tumbo.


Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na;



  1. Kuchoka choka sana bila sababu maalum
  2. Kuuma mgongo au kiuno
  3. Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia
  4. Kizunguzungu
  5. Kukosa usingizi
  6. Usingizi wa mara kwa mara
  7. Maumivu makali sehemu ya mwili
  8. Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali. Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali
  9. Kichefuchefu
  10. Kiungulia
  11. Tumbo kujaa gesi
  12. Tumbo kuwaka moto
  13. Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
  14. Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
  15. Kutapika nyongo
  16. Kutapika damu au kuharisha
  17. Sehemu za mwili kupata ganzi
  18. Kukosa hamu ya kula
  19. Kula kupita kiasi
  20. Kusahahu sahau na
  21. Hasira bila sababu.

Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.