IBADA YA LEO JUMAPILI 13/11/2016 KATIKA KANISA LA KKKT USHARIKA WA EBENEEZER KANISA KUU SHINYANGA
Katika ibada ya leo, katika kanisa la KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA (KKKT) usharika wa Ebeneezer kanisa kuu Shinyanga imekuwa njema sana kwani ilikuwa ni ibada iliyojaa utukufu kwa kupata neema ya kuwa na wageni mbalimbali hususan kwaya ya Vijana kutoka Dayosisi ya kaskazini kati usharika wa ILBORU mkoani ARUSHA.
Pia tulipata chakula cha kiroho kutoka kwa Mwalimu JOEL. Y. MKEMWA, kichwa chake cha somo kikiwa ni "WATU WALIOIBIWA" kutoka kitabu cha ISAYA 42:22 " Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa, wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza, wamekuwa mawindo wala hapana aokoaye, wamekuwa mateka wala hapana asemaye, Rudisha."
Katika somo hili mtumishi wa Mungu nabii Isaya anaeleza kuwa mtu anaweza akaibiwa na kuwekwa mateka pasipo yeye kujua, ndio maana unasikia ushoga umeenea dunia nzima na unapewa support na madhehebu mbalimbali, hii ni kumaanisha kuwa watu wameibiwa na kutekwa na kuwekwa magerezani pasipo wao kujua. Nguvu yote hiyo inayotumika ni ya utawala wa kishetani. Mtu anaweza kuja kanisani kila siku na akiwa mwimbaji mzuri lakini kumbe ameibiwa yuko chini ya utawala wa kishetani.
Kitu ambacho kinaibiwa kwa mtu ni nafsi na nafsi ikiibiwa inapelekwa mahali na kuwa msukule.
Misukule ipo ya aina tatu,
1. Msukule wa picha
Mtu anapokufa anakuwa maiti, ile maiti unaiona kama maiti kumbe ile sio maiti bali ni picha tu inayoonekana katika macho ya wanadamu, huyo mtu anakuwa ameibiwa.
2. Msukule wa nafsi
Katika hali ya nafsi, mtu anapokufa nafsi yake inachukuliwa na kwenda kutumikishwa, hao watu ndio wanakuwa wanatumiwa kichawi katika kufanya kazi mbalimbali zilizo ngumu, ndio maana mtu unaweza kumuona analima na akalima eneo kubwa mpaka watu wengine wanashangaa. Kumbe huyo mtu hafanyi hiyo kazi peke yake, badala yake anatumia misukule kulima shamba Lile.
3. Msukule wa uzezeta
Kwa msukule wa uzezeta unakuta mtu ameibiwa amefanywa kuwa zezeta kwa ajili ya kumtajirisha mtu mwingine. Matajiri wengi sana wanawafanya watoto wao au ndugu zao kuwa mazezeta ili kujipatia utajiri wa mali.
Hawa watu ni walioibiwa. Pengine hata wewe umeibiwa na kutekwa na kuwekwa magerezani lakini wewe haujiujui kama umetekwa. Unakuta mtu ni mlevi kupindukia mpaka umchukia, Kumbe mtu yule ametekwa. Au Unakuta binti au kijana ameanza uzinzi nawe mzazi ndio unakuwa mkali kiasi cha kuanza kumuadhibu huyo mtu, hiyo sio suluhu ya mtoto wako bali tafuta kujua ni nani aliyemteka ndipo uweze kumkomboa. Yesu alikuja akatufia msalabani, yupo kwa ajili ya kuokoa kilichopotea. Mungu alibariki neno lake Ameen!
Pia katika ibada hiyo, ilihudhuriwa na Baba Askofu Dr. Emmanuel Joseph Makala, Askofu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (DKMZV)
Baba Askofu alitoa salaam mbalimbali kwani ni kipindi kirefu sasa amekuwa katika ziara mbali mbali ndani na nje ya nchi (Ujerumani).
Katika salaam zake ametoa msimamo wake juu ya ndoa za jinsia moja kwa jinsi dunia nzima, wachungaji na maaskofu wengine wanavyolipokea.
Askofu alisema jambo hili hatalikubali wala kulipokea.
Pia katika ibada hiyo, ilihudhuriwa na Baba Askofu Dr. Emmanuel Joseph Makala, Askofu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (DKMZV)
Baba Askofu alitoa salaam mbalimbali kwani ni kipindi kirefu sasa amekuwa katika ziara mbali mbali ndani na nje ya nchi (Ujerumani).
Katika salaam zake ametoa msimamo wake juu ya ndoa za jinsia moja kwa jinsi dunia nzima, wachungaji na maaskofu wengine wanavyolipokea.
Askofu alisema jambo hili hatalikubali wala kulipokea.
Askofu Dr. Emmanuel Joseph Makala akitoa salaam Ibadani
Mchungaji msaidizi wa Dean wa usharika JACKSON MAGANGA akiwakaribisha wageni kutoka Arusha kwa niaba ya Dean ambaye yuko safari mkoani Kilimanjaro
Katibu wa Usharika wa Ebeneezer kanisa kuu Shinyanga IBRAHIM ALFRED LYANGA akisoma matangazo wakati wa ibada
Katibu wa Usharika Ibrahim Lyanga (kushoto), Mwimbaji Laurens kutoka Dar es salaam wapili kutoka kushoto, Mwalimu Bathalomayo Mtenga (katikati),mwenyekiti wa kamati ya uinjirist mkoa wa Dar es salaam mwenye shati jekundu na Fred Shoo (kulia) wakifuatilia ibada kwa makini.
Mwalimu Joel Y. Mkemwa (kulia), mwinjilisti wa mtaa wa mjini Ebenezer Kanisa Kuu ELISHA SWAI (katikati) na mchungaji msaidizi wa Dean kanisa kuu (kushoto)
Askofu Dr. Emmanuel Joseph Makala (kushoto), Mama Askofu (katikati) na mwanafunzi wa uchungaji Tumaini Msengi
Mwenyekiti wa kwaya ya Vijana ya Ilboru Arusha, MPONJOLI MWAKABIBI akitoa salaam kwa Usharika na kutambulisha wanakwaya kutoka Arusha
Kwaya ya Vijana kutoka Dayosisi ya kaskazini kati wakiimba ibadani
Wanakwaya kutoka Arusha wakiimba
Wakati wa kuagana nje mara baada ya ibada
Wanakwaya kutoka Arusha wakiwa nje mwishoni kabisa mwa ibada
MARA BAADA YA IBADA KUISHA WAGENI WALIPATA CHAKULA CHA KIMWILI, JIONEE PICHA ZIFUATAZO HAPA CHINI
Karibuni kwa chakula
Wageni kutoka Arusha wakipata chakula
Chakula kitamu sana
Wakiwa katika harakati zile zile
Hawa nao wakiwa na mwenyeji wao, mwanafunzi wa uchungaji Tumaini Msengi
Kwa kweli hata sisi tuliwafurahia hawa wageni
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi