YANGA YAILAZA NJAA MBAO FC 3:0


KOCHA Mhoalanzi wa Mholanzi Franciscus Johannes ‘Hans’ van der Pluijm amerejea na mguu mzuri baada ya leo kuiwezesha timu hiyo kuendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.  

Kwa ushindi huo uliotokana na mabao ya beki Mtogo, Vincent Bossou, viungo Mkongo Mbuyu Twite na mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe, Yanga inafikisha pointi 27 baada ya mechi 12 ikiendelea kushika nafasi ya pili, nyuma ya Simba SC yenye pointi 32 za mechi 12 pia. 


Ijumaa Yanga ilimuandikia barua ya kumuomba kurudi kazini kocha Pluijm, aliyejiuzulu mapema wiki hii baada ya kukerwa na uongozi wa klabu kuleta kocha mpya, Mzambia George Lwandamina bila kumtaarifu, akisema huko ni kumvunjia heshima.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.