Picha: Samaki mkubwa aliyekutwa ufukweni amekufa
0
Samaki mkubwa amekutwa amekufa katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Bandari ya Kilwa, Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa samaki huyo alianza kuonekana kuanzia juzi akielea baharini lakini hawakujua kama alikuwa amekufa hadi Jana aliposukumwa hadi kwenye ufukwe wa bahari.
Wakazi hao wanaeleza kuwa samaki huyo ana urefu wa futi 30.