KUELEKEA DERBY YA KARIAKOO…BOKA AFUNGUKA SIRI YA UBORA WAKE YANGA…



Beki wa Yanga SC, Chadrack Boka, amefichua siri ya kiwango chake bora uwanjani, akisema kuwa kufuata maelekezo ya kocha wao, Hamdi Miloud, wakati wa mazoezi kumemsaidia sana. 


Boka, ambaye aliifungia Yanga bao lake la kwanza tangu kuwasili Tanzania, alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji FC katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Akizungumza kuhusu kiwango chake, Boka alisema kuwa umakini wake katika kufuata maelekezo ya benchi la ufundi umemsaidia sana. Aidha, alibainisha kuwa baada ya mazoezi rasmi ya timu, hutumia muda wa ziada kufanya mazoezi binafsi ya kupiga mipira ya faulo.


“Mashabiki wa Yanga hawakutarajia kwamba nitafunga kwa mpira wa faulo, lakini ukweli ni kwamba natumia muda wangu wa ziada kufanya mazoezi ya kupiga mipira hiyo, nikiwa na kipa,” alisema Boka.


Kuhusu ushindani wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Boka alieleza kuwa msimu huu ligi imekuwa ngumu, kwani kila timu inapambana kutafuta pointi tatu muhimu. Hata hivyo, alisisitiza kuwa Yanga inaendelea kupambana ili kuhakikisha inafikia lengo lake la kutwaa ubingwa msimu huu. 

Post a Comment

Previous Post Next Post