SIMBA WATAMBULISHA KOCHA MPYA WA MUDA, AUNGANA NA TIMU KWENDA MALAWI


KLABU ya Simba SC imemtangaza Juma Mgunda kuwa Kocha Mkuu wa muda wa Klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi, Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Kocha Mgunda ataongozana na kikosi hicho katika safari ya Leo kuelekea Malawi kwaajili ya kushiriki Mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets ya nchini humo.

Aidha Mgunda atasaidiana na Kocha msaidizi Selemani Matola katika mechi zote ambazo Simba itashiriki kwenye kipindi hiki ambacho klabu inaendelea kutafuta Kocha Mkuu.

Uongozi wa klabu ya Simba umesema kuwa unaushukuru Uongozi wa Klabu ya Coastal Union kwa kumruhusu Kocha wao Juma Mgunda kujiunga na Klabu hiyo kwenye kipindi hiki cha mpito.

Kocha Juma Mgunda ni Kocha mwenye Leseni A ya CAF ambae anakidhi vigezo ya kuiongoza timu kwenye mashindano ya yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Kikosi Cha Simba kinataraji kuondoka nchini Leo Alhamisi ya September 08,2022 kuelekea Malawi kwaajili ya mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets, Mchezo utakaopigwa September 10,2022 kuanzia majira ya saa 10:00 Jioni.

Post a Comment

Previous Post Next Post