ALI KIBA AKUTWA NA MAAMBUKIZI YA KORONA (UVIKO - 19), SHOO ZAKE MAREKANI ZAAHIRISHWA


MSANII nguli wa mziki wa kizazi kipya(Bongo fleva), Alikiba ameelezea masikitiko yake baada ya kulazimika kuahirisha shoo zake alizozipatia jina la ‘The Only One King’ zilizotazamiwa kuanza Septemba 2, mwaka huu katika majiji mbalimbali nchini Marekani.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa instagram Alikiba amwelezea sababu kubwa iliyopelekea kuahirishwa kwa shoo hizi ni baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya korona baada ya kufanyiwa vipimo vya awali.

Amekutwa na maambukizi ya virusi vya korona baada ya vipimo vya awali

Katika ujumbe wake huo aliandika “Nimelazimika kusimamisha shoo zaku na kubadilisha ratiba pia haraka iwezekanavyo. Afya ya bendi yangu, watu wangu ninao ambatana nao na nyie mashabiki ni muhimu kuliko kitu kingine chochote”
Awaomba radhi mashabiki zake kwa usumbufu

Ameendelea kwa kuwaomba radhi mashabiki zake kwa usumbufu uliojitokeza na atatoa ratiba mpya muda mfupi ujao.

Imeandikwa:Simon Molanga kwa msaada wa mitandao

Post a Comment

Previous Post Next Post