
Kikosi cha Simba kilifanya mazoezi yake ya mwisho jana jioni katika Uwanja wa Namfua tayari kuwakabili Singida United leo
Kocha wa Simba Mfaransa Pierre Lechantre alisema mechi haitakuwa ngumu kutokana wameshachukua ubingwa tayari wa Ligi Kuu Bara msimu huu na hiyo ndio alikuwa dhamira yao kubwa.
"Tunaweza kupoteza kutokana na wachezaji kufanya mazoezi wakiwa na furaha ya ushindi kuliko mechi ya kesho na yakatokea kama ya Manchester City wameuchukua ubingwa wakafungwa na timu ndogo, sisi hatuwezi kubweteka na kombe " alisema.
"Tunatambua Singida siyo timu ndogo na tumejipanga kuhakikisha tukapata ushindi katika mechi ya kesho," alisema Lechantre ambaye aliongezea kuwa timu yake haitakuwa na mabadiliko yoyote ya kikosi.
"Tutacheza Kikosi kamili ili kuhakikisha tunashinda mechi na Singida United, " alisema Lechantre.
Tags:
michezo