ALICHOKISEMA HAJI MANARA BAADA YA SIMBA KULAZIMISHWA SARE NA LIPULI FC

Baada ya Simba kubanwa na kulazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Lipuli kwenye uwanja wa Uhuru, afisa habari wa klabu hiyo Haji Manara amesema, siku zote mpira hauna matokeo rafiki, wakati unapohitaji ushindi unapata matokeo usiyoyatarajia.

“Mchezo wa mpira hauna matokeo rafiki siku zote, wakati unapotarajia kushinda ndio hivyo mnatoka-draw katika timu ambayo kwa kweli tulitarajia tutashinda, kikubwa mimi niwaombe tutulie, sasa hivi akili zetu tunazielekeza katika mkutano wa December 3 na ajenda tumeshazito. Ajenda kubwa ni kamati ya zabuni itamtangaza aliyeshinda tenda ya kununua hisa za (asilimia 50) za Simba.”

“Najua mashabiki wetu wamesikitishwa na matokeo ya mechi ya leo, mimi binafsi, mashabiki wote na viongozi na viongozi wote hatukutarajia matokeo ya leo. Lakini kama walivyosema walimu huo ndio mpira.”

Post a Comment

Previous Post Next Post