Mshindi wa kwanza kitaifa katika matokeo ya mitihani ya kidato cha
nne mwaka 2016 Alfred Shauri amesema ndoto yake ni kuwa mhandisi wa
umeme wa viwanda.
Alisema hayo jijini Dar es Salaam alipotembelea ofisi za kampuni ya
magazeti ya serikali (TSN) inayochapisha magazeti ya ya DailyNews,
SundayNews, Habarileo, Habarileo Jumapili na SportLeo.
"Ndoto yangu ni kuwa mhandisi wa umeme wa viwanda ili kutengeza
mashine za viwanda, natarajia kuwa mwekezaji wa viwanda afrika," alisema
Alfred.
Aliwashauri vijana kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa ya maendeleo.
CHANZO - HABARI LEO
Tags:
habari